The world of mesut oźil
Wakati dunia ya leo kama ukimuuliza mtu akutajie viungo bora aliowahi kuwashuhudia atakutajia iniesta,xavi,modric, KDB au Pogba n.k lakini kuna mtu mmoja asikiki sana masikioni mwa watu ni moja kati ya viungo na kipaji bora kabisa yani kuwahi kuubariki mpira barani ulaya na huyu si mwingine ni Mesut ozil
Mesut ozil ndie mchezaji pekee duniani katika historia ya mpira wa miguu kuwa Top assist katika premier league,akiwa na klabu ya Arsenal,Top assist Bundesliga akiwa na klabu ya Werder Bremen,Top assist la Liga akiwa na Real Madrid,Top assist Champions league akiwa na Real Madrid,Top assist Europe league akiwa na Arsenal,Top assist EURO CUP akiwa na German na Top assist World cup akiwa na German national team
Mesut ozil ni mchezaji ambaye watu hawamzungumzi sana lakini ameonesha ubora mkubwa sana ambao ulimfanya kila mtu atamani kuwa nae kwenye timu, Mesut ozil amefanikiwa kubeba German cup DFB-pokal akiwa na Werder Bremen kwa kuwafunga Bayern Leverkusen,pia ametwaa Copa de Rey na la Liga akiwa na Real Madrid na FA cup ya Uingereza 4 akiwa na Arsenal pia ni mshindi wa kombe la dunia pale Brazil 2014 akiwa na timu ya taifa ya German
Pia Ozil ndie mchezaji pekee wa timu ya taifa ya German ambaye ameshinda tuzo nyingi za mchezaji bora wa mwaka wa ujerumani
Mesut ozil amezaliwa October 15,1988 huko Gelsen kirchen, ujerumani amechezea timu kama schalke04, Bremen, Madrid, arsenal,fenerbahce na beskitas
Youth career ya Ozil
1995-1998 West falia 04Gilsen kirchen
1998-1999 Teutonia schalke-Nord
1999-2000 Falke Gelsen kirchen
2000-2005 Rot-weiss Essen
2005-2006 Schalke04
Senior career
2006-2008 Schalke04
2008-2010 Werder Bremen
2010-2013 Real Madrid
2013-2021 Arsenal
2021-2022 Fenerbahce
2022-retire Beskitas
National team career
2006-2007 German u-19
2007-2009 German u-21
2009-2018 German senior team
Maoni
Chapisha Maoni